Karibu!

Tafadhali nisikilize ninachotaka kuwaelezeni watu wote wa Tanzania na wa Afrika Mashariki. Ugojwa wa kiharusi unahitaji matibabu ya haraka. Utajuaje kwamba mtu amepata kiharusi? Soma hapa!

Utajuaje kwamba mtu amepata kiharusi?

English-Swahili Initial symptoms - Dalili za awali
Hemi limb weakness, numbness/acroparesthesia – udhaifu wa ungo, kufa ganzi/msisimko wa viungo
One angle of the mouth droops – upande moja wa mdomo unalegea
Visual disturbances – tatizo katika kuona
Speech becomes slurred or words are not found – kuongea kwake ni kwa shida, pia anasahau maneno au anachotaka kukiongea.
Hemiplegia – kupooza kwa paande moja wa mwili
Nerve damage - madhara ya neva
Paralysis- upooza/kipoza
Loss of balance - ukosefu wa usawa wa kutembea pamoja na kuhisi kizunguzungu.

Unapogundua kwamba mtu ana dalili za kiharusi, ni vyema kumpeleka hospitali haraka iwezekanavyo.
Huko hospitalini, ni vizuri kupewa matibabu ya haraka. Manesi na madakitari wanahitaji kumpa moyo huduma nzuri mtu aliyepata kiharusi. Pia marafiki wanahitaji kumpa moyo mgojwa. Hata hivyo mgojwa anahitaji kufanya mazoezi mwenyewe.

Labda usifikiri kwamba kupata nafuu baada ya kiharusi ni mpango wa Mungu tu (Mungu akipenda, Inshallah). Kumbuka kufanya mazoezi ili upate nafuu kwa haraka.
Kwa mfano mimi Baba Yakubu, baada ya kupata kiharusi mara mbili, pia nimefanyiwa operesheni ya moyo, nikaanza kufanya mazoezi kwa wingi, mazoezi ya kukimbia. Nimekimbia marathon (kilomita 42) miaka mitano baada ya kiharusi.
Kwa hiyo nataka kukuambia kwamba inawezekana kuwa imara kimwili baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi. Lakini unahitaji kufanya mazoezi ya mwili, ubongo, moyo na kadhalika.
Kama ndio umepata kiharusi, nakutakia safari njema upate nafuu mapema na kujenga mwili wako vyema tena.
Asante kwa kusoma hadithi yangu! Unaweza kuchangia maoni yako kwa Kiingereza kupitia email yangu: babayakubu43(a-t-sign-here)gmail.com

© Copyright 2021 Kiharusi - All Rights Reserved